About us

KeroYako.Com, ni mradi unaolenga katika kuwashirikisha Watanzania, ndani na nje ya nchi, kuibua na kuyaweka hadharani matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo katika maisha yao ya kila siku, ambayo yanatokana na uwajibikaji duni na usio na tija wa wahusika walioko katika ngazi za kufanya maamuzi.

Mradi huu utakuwa ukihusisha teknolojia za kisasa na zilizo rahisi sana, hivyo kuweza kuwafikia na kufikiwa na mamilioni ya Watanzania, ili waweze kuibua kero zao na kuziweka hadharani, wenye kustahili kuchukua hatua wazisikie na kuchukua hatua stahiki.

Mradi huu hauhusiani na chama chochote cha kisiasa, dhehebu lolote la kidini, au kikundi chochote cha wanaharakati. Ni mradi ambao umelenga kukushirikisha wewe msomaji katika kuuendeleza kwa kuweka kero zilizoko mahali unapoishi au kufanyia kazi.

Kujua namna ya kushiriki katika kuibua, kujadili na hata kutatua kero za Watanzania, kupitia Kero Yako, tembelea ukurasa wa mawasiliano yetu
    Blogger Comment
    Facebook Comment