KUONGEZEKA KWA UCHAFU JIJINI DSM


Mimi ni mtanzania tena ninaishi hapa Dar es Salaam, kero yangu kubwa tena inayonisumbua ni hali ya uchafu kuzidi kukidhiri maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam. Kiukweli nikiwa kama mtanzania siwezi kujisifia kwa hili maana nchi yangu kwa ujumla ni chafu.

Hebu tujiulize kwa nini maeneo mengi ukipita utakuta viroba vya uchafu vipo rundo kwa marundo ina maana hakuna watu wanaoshughulikia na haya maswala ya usafi katika mitaa yetu au katika serikali za mitaa hakuna kamati za usafi??? Watanzania tunatakiwa kujirekebisha utakuta mitaro imejaa taka mvua zikinyesha maji hayatembei wananchi wanaokaa maeneo hayo wanailalalmikia serikali, swali je magonjwa ya milipuko kwa watoto hasara inakuwa kwa nani serkali au ninyi mnakaa hayo maeneo??.

Inauma sana tena inasikitisha kuona njiani unakutana na rundo la mauchafu tena hasa mifuko ya nailon, pampas zilizotumika hata pad za wanazotumia akina mama zimezagaa mitaani jamani watoto wetu tunawafundisha nini kwenye swala la usafi.

Sasa imefikia mpaka uchafu unatupwa barabarani, watanzania tujiangalie mara mbili hakuna mtu anayeweza kuja kukufanyia usafi maeneo yako kama sio wewe mwenyewe kufanya hivyo.

Serikali ichukue hatua kwa maeneo yote yanayotupwa uchafu na kila mtu awe mlinzi wa mwenzake katika suala nzima la kulinda mazingira yetu tuishio, hii itaweza kusaidia walau kidogo na ikumbukwe usafi huanzia tangu utoto na tukiwafundisha watoto wetu jinsi ya kuwa wasafi na maeneo yetu nadhani vizazi vijavyo vitakuwa na hiyo karama ya usafi na sio uchafu.
Share on Google Plus
    Blogger Comment
    Facebook Comment

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment