Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Sikilizeni Kero Hii


Mimi kama mzazi kero yangu kubwa ni ongezeko la ombaomba hasa watoto wadogo wa kuanzia miaka 4 -13 barabarani tena wakiwa wamebeba watoto wenzao wadogo zaidi yao. Hili ni tatizo na ni aibu kwa Tanzania hasa ofisi husika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, kama sijakosea ofisi hii inamilikiwa na Mh Sophia Simba ambaye ni mwanamke tena kama sikosei ni mzazi, hivi hili jambo halioni au ndio kulifumbia macho??


Mimi ninachojua wizara kama wizara lazima iwe na fungu la kuwasaidia au kuwafanya hao watoto au ombaomba wasiwepo tena kwenye barabara zetu, kwanza ni risk sana magari yanapita kwa kasi na yanaweza kusababisha hata ajali, hata hivyo vipi suala la watoto kufanyiwa vitendo viovu kama kubakwa na kunajisiwa nyakati za usiku hili waziri halioni au ndio kaziba masikio??. Naamini kabisa fungu lipo tena la kutosha kuwawezesha hawa watu wasiwepo tena mabarabarani.


Sitaki kuamini kwamba wizara imeshindwa kuwaondoa hawa watoto nilichokiona ni kwamba wazazi wa hawa watoto huwa wanakaa sehemu na kuwatuma watoto wao waende kuomba, sasa kama mzazi ni mzima tena anaweza kufanya chochote kwa nini wizara isitunge sheria ya kuwaadhibu hao wazazi wanao watuma watoto kuomba pesa nyakati ambazo wanatakiwa kwenda shule au kuwa mahala salama??


Mh Waziri mwenye mamlaka ya wizara husika jitume kuondoa hili bomu la watoto wa mitaani tunaona ni jinsi gani watoto wadogo wanavyoingia kwenye vitendo viovu na hasa hili janga la makundi ya kigaidi na mengineyo je wakijiunga huko kwa malipo ya chakula na malazi watanzania tutasema wameisaliti nchi? maana baadae lazima watakuja kufanya unyama kwenye nchi wanayotoka, hebu tuache kujibweteka kama unapopewa ofisi basi jitahidi kuifanyia haki na sio vinginevyo.


Mimi kama mzazi nitaendelea kuilaumu ofisi husika maana sioni kama imewajibika vya kutosha kuhusu swala hili.
Share on Google Plus
    Blogger Comment
    Facebook Comment

Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. kwakweli ili limeshakuwa tatizo haswa

    ReplyDelete