Wakazi wa Mloganzila, Kata ya Kwembe, Wilayani Kinondoni waandamana Ofisi za Wizara ya Ardhi

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki  akizungumza na baadhi ya wananchi wa Mloganzila, Kata ya Kwembe, wilayani Kinondoni katika Ofisi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi juu ya kudai fidia za maeneo yalichukuliwa katika Mradi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kufatilia Madai  kwa  Wakazi  wa Mloganzila, Kata ya Kwembe, wilayani Kinondoni, Fedrick Schone akitoa malalamiko yao katika Ofisi za wizara ya  Nyumba na Maendeleo ya Makazi kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akisikiliza madai ya wananchi wao leo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki amesema madai yao watashughulikia ndani ya siku saba kwa kwenda kuzungumza na wananchi hao baada ya kujadili na Waziri wake. Picha na Emmanuel Massaka
Share on Google Plus
    Blogger Comment
    Facebook Comment

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment