Mh Amos Makalla aridhia pendekezo la wananchi wa jimbo lake kumuona Waziri Mkuu

Mbunge wa mvomero Mh Amos Makalla akimpa pole na Fedha za matibabu mmoja wa wakulima aliyejeruhiwa kwa kuvunjwa Mkono.


Mbunge wa Jimbo la Mvomero mkoani Morogoro, Mh Amos Makalla ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, ameridhia pendekezo la wananchi wa jimbo lake kumuona Waziri Mkuu, Mh Mizengo Pinda kufuatia mapigano ya wakulima na wafugaji yaliyotokea wiki iliyopita ambapo watu watatu walipoteza maisha huku wengine wengi wakijeruhiwa baada ya wafugaji kulishia mifugo yao kenye Mazao ya wakulima katika mashamba yaliopo bonde la mgongola.

Kutokana na hali hiyo Mbunge kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama waliitisha mkutano wa hadhara kijiji cha Kugugu kuongea na wakulima wanaolima katika bonde la mgongola pamoja na mambo mengine wananchi walimuomba Mbunge wao kuundwe Kamati ya kumuona Waziri Mkuu kuhusiana na mipaka ya bonde la Mgongola ambalo limekuwa Mahakamani kwa zaidi ya miaka 15 na machafuko ya mara kwa mara yametokana na bonde hili kwa wafugaji wa kijiji cha Kambala kulishia mifugo yao kwenye Mazao ya wakulima na kupelekea uvunjifu wa Amani wa mara kwa mara.

Akiongea kwa niaba ya wananchi mkazi wa kigugu ndugu Salihina Mpenda alisema kuwa kesi ya bonde la mngongola umekuwa muda mrefu serikali haichukui hatua  watu wanaendelea kufa kila kukicha imefika wakati jitihada zako Mbunge ulizozifanya kuwaleta mawaziri 4, barua ulizomuandikia Waziri Mkuu na Waziri wa ardhi sisi wananchi tunakupongeza ila inapaswa tukuongezee nguvu tukamuone Waziri mkuu.

Akijibu hoja hiyo Mbunge na Naibu Waziri aliridhia ombi lao la kuundwa Kamati ya wakulima ya kumuona Waziri mkuu na akawataka wachague watu kumi na yeye kama Mbunge atagharamia gharama zote.

Aidha kwa upande mwingine Mkuu wa Wilaya hiyo, Mh Festo Kiswaga amewahakishia hali ya usalama ndani ya bonde la Mgongola ni shwari wakulima waendelee na shughuli na Ulinzi wa Askari wa doria umeimarishwa.
Share on Google Plus
    Blogger Comment
    Facebook Comment

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment