Mgogoro wa Ardhi maeneo ya Chanika Nyeburu jijini Dar es Salaam, Wahusika Sikilizeni Kero Hii

Kero yangu ni kwa watu wa Maliasili kutoka Kisarawe kwenda kufanya uharibifu kwenye mashamba yetu yaliyopo Chanika kijiji cha Nyeburu eti wakidai ni sehemu ya hifadhi ya maliasili, Sisi tulinunua mashamba hayo kupitia serikari ya mtaa na tulihakikishiwa kwamba hakuna tatizo lolote kwenye hiyo ardhi, sisi tulishangaa sana kuona uharibifu umefanywa na watu wa maliasili bila kufuata utaratibu.

Tunaomba waziri wa ardhi aingilie huu mgogoro sababu tunashindwa kufanya shughuli zetu za kilimo kuhofia kutokea tena uharibifu.

Tunaomba watu wa maliasili na wahusika kwenye sekta ya Ardhi watuonyeshe mipaka ya hifadhi kwa kutumia ramani ya mwaka 1954 iliyopitishwa kisheria.
Share on Google Plus
    Blogger Comment
    Facebook Comment

Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.