MAKONDA AKUTANA NA WANANCHI WA KAWE MZIMUNI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wananchi wa Kawe Mzimuni alipofika kutatua mgogoro wa ardhi kati yao na  taasisi moja ya kiislamu inayomiliki Shule ya Sekondari ya Seminari ya Qiblatain D $B iliyopo eneo hilo Dar es Salaam leo asubuhi.


 Katibu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa eneo hilo Mgili Wambura alimwambia DC Makonda kuwa eneo hilo tangu zamani ilikuwa ni barabara hivyo wanashangaa kuvamiwa hivyo alimuomba Makonda kusaidia kuondoa mvutano huo.

Mmoja wa wakilishi wa shule hiyo ya Sekondari ya Seminari ya Qiblatain D $B,  Hamad Iddi Almas alimwambia DC Makonda (hayupo pichani), kuwa eneo hilo linamilikiwa na taasisi yao tangu siku nyingi.
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.

Wananchi wa Kawe Mzimuni wakiwa kwenye ukuta walioubomoa kutokana na kujengwa eneo la barabara.Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda amezitaka pande mbili zinazogombania ardhi maeneo ya Kawe Mzimuni kufika na vielelezo vya umiliki wa eneo hilo ili kumaliza mgogoro huo.


Mwito huo ameutoa wakati akizingumza na wananchi wa eneo hilo Dar es Salaam leo asubuhi ambao walijichukulia sheria ya kubomoa ukuta uliojengwa na mwananchi mmoja wa eneo hilo kuwa ulijengwa kwenye barabara.

Mbali na kubomoa ukuta huo wananchi hao wanavutana  la taasisi moja ya dini ya kiislamu inayomiliki Shule ya Sekondari ya Seminari ya Qiblatain iliyopo eneo hilo kuwa imemega eneo la Shule ya Msingi ya Ukwamani.

"Nimekuja hapa baada ya kusikia mgogoro uliopo wa kugombea ardhi nafikiri ofisa mipango mji wa Manispaa alifika hapa kuzungumza nanyi naomba baada ya siku saba pande zote zinazovutana zije na vielelezo ofisini kwangu hapo tutajua nani mmiliki wa eneo hilo" alisema Makonda.

Katibu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa eneo hilo Mgili Wambura alimwambia Makonda kuwa eneo hilo tangu zamani ilikuwa ni barabara hivyo wanashangaa kuvamiwa hivyo alimuomba Makonda kusaidia kuondoa mvutano huo.

Mmoja wa wakilishi wa shule hiyo ya Sekondari ya Seminari ya Qiblatain Hamad Iddi Almas alimwambia Makonda kuwa eneo hilo linamilikiwa na taasisi yao tangu siku nyingi jambo lililosababisha wananchi kuanza kuzomea wakipinga umiliki huo.
Share on Google Plus
    Blogger Comment
    Facebook Comment

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment